SERIKALI YAENDELEA KUFUNGUA MIKOA KIUWEKEZAJI



#KAZIINAONGEA

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kufungua njia za uwekezaji nchini, ikiwemo  mkoani  Dodoma ambako Kiwanda cha kuzalisha mafuta ya kupikia cha Mainland kinajengwa. 

Mradi huo wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya kupikia, unaojengwa  mkoa humo, umeonyesha maendeleo chanya tangu uliposajiliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) mwaka 2023. Ni Mradi wenye mtaji wa dola za Kimarekani milioni 60, unaotarajiwa kuanza rasmi uzalishaji mwaka huu 2025.  

Aidha, ujenzi huo na ufungaji wa vifaa vimefikia asilimia 90, ambapo kukamilika kwa mradi huu kutatoa ajira kwa watu 500, hatua inayochochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Dodoma na maeneo ya jirani.

TIC imeonyesha umuhimu wa huduma zake kwa kuhakikisha wawekezaji wanapata msaada wa haraka kusajili miradi yao na kuanza utekelezaji kwa wakati. Hii inasaidia kupunguza ucheleweshaji wa miradi ya maendeleo na kuvutia uwekezaji zaidi nchini Tanzania.

Kupitia juhudi hizi, Dodoma inazidi kuwa kitovu cha uwekezaji, ikithibitisha kuwa mazingira rafiki ya uwekezaji yanaweza kuleta matokeo ya haraka na yenye tija.

*#KAZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments