SERIKALI imetoa Bilioni 20 kwa ajili ya malipo ya fidia kwa wakazi zaidi ya 200 wa Kata kipunguni Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Haya yamebainika leo mapema Jijini Dar es Salaam wakati wa Halfa ya makabiziiano ya fedha kwa wananchi wa kata hiyo ,katika halfa hiyo kulishudiwa na ,Mbunge wa Jimbo Segerea pamoja na waandishi wa habari.
Akizungumza kwenye halfa hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Viwanja vya ndege nchini (TAA) Abdul Mombokaleo, amesema fidia hizo zitatoka kwa awamu mpaka kukamilisha idadi ya wakazi wa kata ya kipunguni 1864.
Amesema lengo la serikali na mamlaka hiyo kila mkazi ambaye amefanyiwa uthamishaji atalipwa fidia.
"Mchakato wa kuwalipa fidia umeanza toka mwaka 1997 na kwa sasa mmeanza kulipwa zote ni jitihada za Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa wakazi wa Kipunguni wanalipwa fidia"Amesema
Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mkuu wa Fedha na Utawala kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini(TAA), Shadrack chilongani, mchako wa kuwalipa wananchi utafanyika mara baada ya wao kujaza fomu ambazo zipo serikali ya mtaa wa kipunguni.
"Mkajaze fomu zile na mkimaliza watu wa Benki watazipitia ndani ya siku mbili fedha zitakuwa zimeingiziwa kwenye Akaunti zenu"Amesema.
Chilongani amewahiza wananchi hao kuharakisha ujazaji wa fomu hizo huku watakapopata fidia waweze kuhama na kupisha maeneo hayo kwa ajili ya uendelezaji wa uwanja wa ndege.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere, Benta Bankwa, amesema baada ya wananchi hao kuhama wamejipanga kwenda kutanua uwanja huo ili ndege kubwa ziwasili nchi.
"Tumepanga kujenga maduka makubwa na ofisi mbalimbali,sehemu ya kuhifadhia mizigo"amesema .
Naye, Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mhe. Bonnah Ladislaus Kamoli, amempongeza Mkurugenzi wa TAA kwa jitihada zake za kuhakikisha wananchi hao wanalipwa fidia.
"Nampongeza sana mkurugenzi amepambana suala hili ,mimi nimeongea naye ofisini kwake kuhusu jambo hili ,pia nampenga Rais Samia kwa kuhakikisha wananchi hawa wamepata fidia."
Pia mwenyekiti wa serikali za mtaa wa kipunpuni, Mwinyijumu Seke,ameipongeza Serikali ya Rais Samia kwa kuwafuta machozi kwa wakazi wa Kipunguni kwa kuwalipa fidia .

0 Comments