Mwenyeki wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Richard Lyimo akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Chama Magomeni, Dar es Salaam.
NA MWANDISHI WETU
CHAMA Cha Tanzania Labour Party (TLP) kimesema hakitashirikiana na Chama chochote kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadaye Mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama hicho Richard Lyimo akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Chama Magomeni jijini Dar es Salaam.
Amesema hakuna Chama chochote nchini chenye nia ya dhati ya kushirikiana na Chama kingine, kwamba vyama vinavyohubiri kuhusu ushirikiano huo vina nia ya kuwalaghai Wananchi.
Lyimo amekumbushia Ushirikiano wa Mwaka 2015 kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ambapo amedai uliwanufaisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) huku vyama vingine vikiishia kufa.
"Suala la vyama kushirikiana nimelisikia, na si mara ya kwanza vyama kutaka kuungana, lakini hakipo Chama ambacho kina nia ya dhati ya kushirikiana, bali vinataka kulaghai Wananchi," amesema Lyimo na kuongeza,
"Ni Muungano ambao Mimi siwezi kuungana, kwasababu hatujawa na vyama vyenye kufanya Muungano wa kweli kukitoa Chama cha Mapinduzi (CCM) madarakani,".
Lyimo amesema kuwa Wakati wa Ushirikiano wa Mwaka 2015 kupitia UKAWA vyama washirika vilikubaliana kuachiana majimbo lakini amedai kuwa hata hivyo CHADEMA ilikiuka makubaliano hayo kwani kiliweka wagombe kwenye majimbo ya wenzake.
Hivyo amesema kama TLP watakwenda kwenye Uchaguzi wenyewe kwani lengo la chama chochote ni kushika Dola na kama Kuna Chama kinataka kuungana nao ni lazima kiiunge mkono TLP kusimamisha mgombea wa kiti cha Urais.
Katika hatua nyingine, Lyimo ameeleza kuwa kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo Chama kitahakikisha kinakamilisha safu za uongozi za mikoa, Wilaya, Kata na ngazi za china kabisa.
Kwamba lengo ni ili viongozi hao wahakikishe wanatafuta wanachama wa kutosha ambao watakiimarisha na kukipa nguvu Chama kuelelea Uchaguzi Mkuu.
Amesema Chama chochote mtaji wake ni wanachama ambao watatoa wagombe katika ngazi mbalimbali za Urais, Ubunge na Udiwani.
.jpg)
0 Comments