#KAZIINAONGEA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kutekeleza ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo katika sekta ya afya ambapo ujenzi wa ghala la kuhifadhi bidhaa za Afya umekamilika kwa asilimia kubwa.
Waziri wa Afya Jenista Mhagama Februari 6, 2025 amekagua ghala hilo la kuhifadhi bidhaa za Afya linalotarajiwa kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Aprili, 2025. Jengo hilo linalojengwa na Bohari ya Dawa kanda ya Dodoma (MSD) lina ukubwa ya Sqm 7,200 na ambalo limegharimu zaidi ya shilingi bilioni 23.7.
*#KAZIINAONGEA*

0 Comments