CHUO CHA VETA SHINYANGA CHATUMIA MAADHIMISHO MIAKA 30 YA VETA KUNADI TUZO KINAZOTENGENEZA, chawaita wadau wa michezo, shule na taasisi mbalimbali zinazohitaji.....




NA MWANDISHI WETU 

CHUO cha Elimu na Ufundi Stadi (VETA) Shinyanga kimetoa wito kwa wadau wa michezo, shule za msingi na sekondari, taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi kutumia Chuo hicho kuwatengenezea Tuzo mbalimbali  (Trophy) ambazo wanaweza kuzitoa kama zawadi kwa watu waliofanya vizuri.

Wito huo umetolewa leo Machi 20, 2025 jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Chuo hicho Abraham Mbuguni akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo wanashiriki kwenye maonesho ya bunifu yanayokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 30 ya Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA).

"Chuo hiki kiko Kanda ya Magharibi, na tuko hapa Dar es Salaam ukumbi wa Mwalimu Nyerere (JNICC)  katika kuadhimisha miaka 30 ya VETA. Na kila Kanda imekuja kwa staili yake. Sisi hapa pamoja na mambo mengi na mazuri tunayoyafanya pale katika Chuo cha VETA Shinyanga, lakini leo hii tumekuja kutangaza bidhaa zetu hizi hapa mnazoziona," amesema Mbuguni na kuongeza.

"Tuna mashine inaitwa CNC (Computer Numerical Control), tunatengeneza Trophy (tuzo) kwa maumbo mbalimbali, tunachora mawe ya msingi, milango, kazi zote za mbao, kazi zote za vioo, kazi zote za mawe ya msingi, Na shughuli hizi tunazifanya kwa ustadi, ndiyo maana mnaona bidhaa zetu ziko tofauti kidogo na nyingine ambazo mmeziona," amesema Mispa na kubainisha kuwa,

"Kahiyo ukija unatupa "Specification" zako na unataka nini, basi mtaalamu wetu ataweka mchoro, ataingia kwenye Computer, basi ataandaa kama ni Trophy kwa namna ambavyo mtakuwa mmeelewana, lakini bidhaa zetu ni kama zinavyoonekana, tunafanya vizuri,".

Mbunguni amesema "Tunatoa wito kwa wadau wa michezo, shule za msingi, shule za sekondari, taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi ambapo mnaweza kutoa tuzo mbalimbali kwa watu waliofanya vizuri. Basi tunaomba mfike VETA Shinyanga ili tuwatengenezee kwa gharama nafuuu, kwahiyo karibuni sana VETA Shinyanga tuwahudumie,".

Akizungumzia kuhusu mafunzo yanayotolewa na VETA Shinyanga Mwalimu Mkuu Mbuguni amebainisha kuwa wana mafunzo ya muda mrefu na mafunzo ya muda mfupi.

Kwamba mafunzo ya muda mrefu ni miaka miwili mpaka mitatu ambapo gharama ya mafunzo kwa mwaka, kwa mwanafunzi mmoja wa Bweni analipa ada ya shiligi 12,000 na kwamba kwa mwanafunzi wa kutwa, analipa ada ya shilingi 60,000 tu kwa mwaka.

"Hivyo tuone ni jinsi gani Serikali ya Jamhuri ya mmungano wa Tanzania inavyowapenda wananachi wake. Gharama ya kumfundishe mwanafunzi mmoja kwa mwaka sio chini ya shilingi laki 8. Lakini mzazi anatoa shilingi 120,000 kwa mwezi, kwahiyo gharama nyingine zote zilizobaki Serikali inatoa Ruzuku (inagharamia)," ameeleza Mbunguni na kubainisha,

"Kwa upande wa kozi za muda mfupi, tunaamini kwamba mdhamini au mfadhili ni mzazi mwenyewe, kwahiyo kidogo ada yake imechangamka,".

Mkuu huyo wa Chuo amebainisha kuwa Chuo kina kozi mbalimbali ikiwemo kozi ya mitambo mizito kwamba kozi hiyo ni ya thamani kubwa.

"Kwa mfano, Chuo chetu cha VETA Shinyanga ndiyo Chuo pekee ambacho kinatoa kozi za mitambo nchi nzima na tunapata wanafunzi kutoka Uganda, Kenya, Burundi, Kongo, Elitria, na sasa tumevuka mipaka mpaka Somalia tunapata wanafunzi," amesema Mbuguni.

Ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa Watanzani kupeleka vijana wao kwenye Chuo cha VETA Shinyanga  ili wapate mafunzo ya ufundi stadi ambayo yanaviwango vinavyostahiki.

Post a Comment

0 Comments