NA ABRAHAM NTAMBARA
KAMPUNI ya Mzuri Afrika na Agrima Afrika Co. Ltd imedhamiria kufanya mapinduzi ya Kilimo nchini Tanzania kwa kuja na Teknolojia ya kisasa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 7, 2025 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Shaaban Mgonja amebainisha kuwa wamekuja na Teknolojia ya MZURI (Mashine) ambayo inarahisisha shughuli za kilimo shambani.
Kwamba kwa Afrika zipo Nchi 50 pekee zenye Teknolojia hiyo ikiwemo Tanzania ambapo ameeleza kuwa asilimia 30 ya Ngano inayolishwa nchini Ukraine inazalishwa kupitia Teknolojia hiyo.
"Mashine hii inauwezo wa kulima, kulegeza ungo, kuchanganya mbolea na kuweka mbegu ardhini, tunazo mashine za aina tatu, tuna ya mita 3 ambayo inauwezo wa kulima eka saba kwa saa, tuna ya mita nne na Mita sita, Teknolojia hii inauwezo wa kurahisisha sana shughuli za kilimo," amesema Mgonja.
Kwamba Kampuni ya Mzuri Afrika inafanya kwa ukaribu na Kampuni ya Mzuri World ambapo amesema kwa Ushirikiano wao wameweza kueneza Teknolojia hiyo Nchini.
Mgonja amesema kuwa baada ya kuona zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania ni wakulima akapambana kuona Teknolojia hii inakuja nchini ili kusaidia kuleta mapinduzi ya Kilimo kwamba mashine hiyo inapanda mazao Jamii ya nafaka pekee.
Ameeleza kuwa ili kuonesha mfano wa mapinduzi hayo ya Kilimo kupitia Teknolojia hiyo, tayari wanashamba la ekari 300 Vigwaza mkoani Pwani ambapo kwa mwaka huu wanatarajia kulima ufura ekari 200 Kwa kutumia Teknolojia hiyo.
Katika hatua nyingine amesema kuwa pamoja na Taknolojia hiyo, Kampuni inazalisha mbolea 11 ambapo Kwa sasa mbolea tisa zinatumika Kwa Kilimo
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mzuri World Marek Rozniak amesema kuwa amesema kuwa mashine hiyo ameamua kuileta nchini kwa ajili ya kusukuma Maendeleo ya Tanzania.
Amesema kuwa Teknolojia hiyo itasaidia kuongeza uzalishaji wa Ngano nchini kwani kwa asilimia zaidi ya 90 ya Ngano inayotumika Nchini imetoka nje ya nchi.

0 Comments