*#KAZIINAONGEA*
*Ni katika kuunga mkono juhudi za Rais Samia
MKURUGENZI wa Hoteli ya Makunduchi Villa na Mlezi wa Taasisi ya Twende Pamoja na Mama Sports Promotion inayoendesha Mashindano ya Samia Cup, Mohammed Haji almaarufu Boss Mo ametoa zawadi kwa Rais Samia.
Zawadi hiyo kwa Rais Samia ameitoa Machi 5, 2025 katika hoteli ya Makunduchi, Ungindoni jijini Dar es Salaam kupitia msaada aliotoa wa viti 100 ambapo kati ya viti hivyo, viti 50 ni vya Halmashauri ya Manispaa Kigamboni na 50 kwa ajili ya watu wenye Mahitaji maalum na Watoto Yatima.
Boss Mo amesema kuwa, lengo la kutoa msaada huo ni kwa ajili ya kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ameongeza na kusema kuwa,
"mama anajitoa sana, mama ni mchapakazi, jasiri, hivyo kwa kupitia mwezi mtukufu na siku ya wanawake inayotarajiwa Machi 8, niseme zawadi hii ni yake mama Dkt. Samia Suluhu Hassan na kwa wenye mahitaji maalum" amesema Boss Mo.
Vilevile ametoa rai kwa wadau wenye moyo wa kuweza kusaidia mambo madogo kama haya, hii inataleta tija ya kumsapoti Dkt. Samia.
*#KAZIINAONGEA*

0 Comments