RAIS DKT. SAMIA KINARA WA AMANI, UPENDO NA MSHIKAMANO


#KAZI INAONGEA

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasisitiza Watanzania wote nchini kuendeleza amani, upendo na mshikamano katika sherehe za siku kuu ya eid.

Rais Dkt. Samia ameyaeleza hayo katika mtandao wake sogozi ambapo ameandika kuwa: Nawatakia nyote kheri ya Sikukuu ya Eid al-Fitr. Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema aliyetubariki kuifikia na kuikamilisha Ibada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan aendelee kutusimamia na kutufanikisha. 

Tusherehekee kwa amani, umoja, upendo na utulivu. Tuendelee kudumu katika ibada na kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kulijaalia Taifa letu umoja, amani na mshikamano; atuepushe na yote yenye nia ya kutugawa na azidi kutujaalia baraka zake.

Aidha amewasihi viongozi wa dini kushilikia msimamo wa imani, udhibiti wa nafsi na kujua wajibu wetu katika kuikuza na kuitunza amani yetu nchini.

Rais Dkt. Samia pia ameomba viongozi wa dini  kuwadhibiti wachache miongoni mwao walio na muelekeo wa kuhubiri na kupandikiza chuki kwa wananchi dhidi ya serikali yao. 

"Ni vyema sote tujue kuwa katika mifarakano na hasama hakuna atakayebaki salama. Nawasihi baadhi ya viongozi wa dini  waache kupandikiza chuki badala yake wahubiri amani, upendo na mshikamano.

Eid Mubarak."

*#Kazi na Utu, Tunasonga Mbele*

Post a Comment

0 Comments