RAIS SAMIA AWAPA TAHADHARI WAGOMBEA WATARAJIWA



*#KAZIINAONGEA*

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan,amewatahadharisha wagombea watarajiwa kuwa makini badala ya kuingia kwenye uchaguzi kwa kubahatisha.

Rais Dkt. Samia ameyasema hayo jijini Dodoma katika ufunguzi wa mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Machi 11, 2025, ambapo  amewataka pia Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya, na viongozi wa Serikali za Mitaa wanaopanga kugombea Ubunge kutoa taarifa mapema.

Aidha, Rais amesema kuwa wagombea hao watakapotoa taarifa mapema, hatua hiyo itawezesha nafasi zao kujazwa mapema na kuepuka kushtukiza wakati wa 
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.

Vilevile ameonya  watakaochelewa kutangaza nia yao wanaweza kupoteza fursa zote, huku waliotangaza mapema wakiwa na nafasi ya kurejea serikalini endapo watashindwa.

*#KAZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments