#KAZIINAONGEA
Katika jitihada za kuimarisha mazingira ya uwekezaji kwa Watanzania, Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imesogeza fursa za uwekezaji wa ndani hususan kwa Watanzania, kwa kutoa huduma bora na kufanya uwekezaji wao kuwa katika mazingira bora.
Kwa kuthibitisha hilo, Machi 24 2025 Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kinafungua rasmi ofisi mpya ya Kanda ya Nyasa katika Mkoa wa Njombe, katika ufunguzi huo mgeni rasmi ni Prof. Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji.
Serikali kupitia TIC inalenga kutoa huduma bora kwa wawekezaji wa ndani na imefanya jitihada kuwasogezea fursa kwa karibu. Ofisi hii itaimarisha zaidi uwekezaji wa ndani na kuleta maendeleo ya kiuchumi katika kanda hii na Taifa kwa ujumla, pia imejipanga kutoa huduma kwa mikoa ya Njombe, Ruvuma, Iringa, na Mtwara.
Katika hafla hiyo ya ufunguzi mgeni rasmi pia atatembelea miradi ya uwekezaji na kuwasikiliza wawekezaji ili kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa wawekezaji wa kanda hii.
# *Kazi na Utu,Tunasonga Mbele*

0 Comments