#KAZIINAONGEA
Tanzania imeweka rekodi nyingine katika sekta ya mawasiliano Afrika Mashariki na Kati kwa kuwa ya kwanza kuwa na maabara ya uidhinishaji wa vifaa vya mawasiliano vya kielektroniki ukanda huu ikiwa ni sehemu ya mafanikio makubwa ya Miaka Minne ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Uwepo wa maabara hii umeiwezesha TCRA kufanya uhakiki wa vipimo vya vifaa vya mawasiliano vya kielektroniki kutoka kwa watengenezaji au mawakala kutoka mataifa mengine.
Faida za uidhinishaji wa vifaa vya kielektroniki ni pamoja na kuhakikisha vifaa vinakidhi viwango kwa usalama wa mtumiaji (afya na usalama), kudhibiti muingiliano wa mawasiliano na kuthibitisha ubora wa kifaa kwa kulingana na viwango vilivyowekwa.
*#Kazi na Utu, Tunasonga Mbele*

0 Comments