RAIS SAMIA: TANZANIA MAMBO NI MOTO, asema imepiga hatua kubwa katika Usawa wa Kijinsia


*#KAZIINAONGEA*

Raia namba moja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa Serikali imepiga hatua kubwa katika kufanikisha malengo ya kuhakikisha kesho bora na njema zaidi kwa vijana wa Kitanzania, wa kike na wa kiume.

Rais Samia ameyasema hayo Machi 8, 2025 katika  kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo Kitaifa imedhimishwa jijini  Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

 Rais Dkt. Samia ameeleza kwamba Tanzania ina mengi ya kujivunia katika kuboresha mazingira yanayohakikisha ndoto ya usawa wa kijinsia inafikiwa nchini.

“Tunapoadhimisha miaka 30 tangu Tamko la Umoja wa Mataifa la Mkutano wa Beijing, miaka 10 ya Malengo Endelevu ya Dunia na miaka 5 ya Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa, ni fursa ya kutathmini mafanikio makubwa yaliyofikiwa na kutambua hatua zaidi zinazohitajika ili kuhakikisha kila msichana na mwanamke hapa nchini anapata nafasi ya kufikia ndoto zake,” amesema Rais Samia.

Pia, ameuhabarisha umma wa Watanzania kuwa, hatua mbalimbali za kisera na kisheria zimechukuliwa na zinaendelea kuchukuliwa ili kupambana na mila kandamizi na ubaguzi dhidi ya wanawake na watoto wa kike.

“Watanzania, wake kwa waume, wameunga mkono maamuzi na hatua mbalimbali za kumwezesha mwanamke, hali ambayo imewezesha nchi yetu kupiga hatua kubwa katika usawa wa kijinsia,” ameongeza.

Aidha Rais Samia amefafanua zaidi juu ya maendeleo yaliyopatikana  zikiwemo hatua kubwa zilizochukuliwa katika sekta mbalimbali  nchini. 

Rais ameainisha  Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ambayo Tanzania inajitahidi kuyapunguza ama kuyaondoa kabisa ambayo ni umaskini,  njaa, kuboresha afya na ustawi katika kukuza ujuzi na utaalam, elimu bora, usawa wa kijinsia katika uongozi na sekta binafsi, maji safi na usafi.

Sambamba suala la nishati safi ya kupikia, ikiwemo umeme na nishati mbadala. Pia
kazi zenye staha, ukuaji wa viwanda, ubunifu na miundombinu, pamoja na kuimarisha amani, haki na taasisi madhubuti.

“Hadi tunapofanya tathmini ya mpango wa tatu wa maendeleo katika Dira ya Taifa ya Maendeleo, tayari tumepunguza umaskini kwa asilimia 26 kutoka kiwango cha awali tulipoanza utekelezaji wa dira. Leo hii, pamoja na jitihada zinazoendelea, tunakaribia kufikia asilimia 30,” amesema.

Vilevile , Rais Dkt. Samia amefafanua kapwa upande wa uhakika wa chakula kuwa Tanzania imejitegemea kwa chakula kwa asilimia 128 na imefanikiwa kuondoa njaa kwa asilimia 100.

Pamoja na hayo Rais Dkt. Samia amewaasa Watanzania wanawake na wanaume kuendelea kujenga jamii makini yenye maadili ya Kitanzania, kuanzia ngazi ya familia, ambayo ndiyo msingi wa Taifa imara.       

*#KAZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments