*#KAZIINAONGEA*
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameshiriki Mkutano wa 50 wa Bodi ya Wadhamini (Governing Council) ya Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB), unakaofanyika jijini Kampala nchini Uganda Machi 13, 2025 katika Hoteli ya Serena.
Dkt. Mwigulu amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Meja Jenerali Paul Simuli na Viongozi wengine Wakuu wa Benki hiyo, akiwemo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya EADB, ambaye pia ni Kamishna wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Benard Mono.
*#KAZIINAONGEA*

0 Comments