ZITTO: TUNATAKA WAJUMBE WA SASA WA TUME YA UCHAGUZI WAONDOKE



NUKUU za Kiongozi Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akizungumza wakati wa kongamano la viongozi Mkoa wa Lindi lenye kauli mbiu ya operesheni linda demokrasia lililofanyika Lindi mjini, Machi 29, 2025:-

 "Tume ya Uchaguzi yenye wajumbe kama Omari Mapuri ambaye amewahi kuwa Mwenezi wa CCM inawezaje kutenda haki kwa watu wote? Sheria ya sasa ya Tume Huru ya Uchaguzi imeweka utaratibu kuwa angalau wajumbe wa Tume ya Uchaguzi wapatikane kwa ushindani. Watu waombe na wafanyiwe usaili. Serikali ya CCM haitaki kutekeleza jambo ambalo wamelitunga wenyewe"- @zittokabwe, Kiongozi wa Chama Mstaafu, ACT Wazalendo.

"Tunataka wajumbe wa sasa wa Tume ya Uchaguzi waondoke. Nafasi zao zitangazwe, watu waombe, tupate wajumbe wapya. Huu umekuwa wimbo wetu tangu mwaka jana. Muda wa kufanya hilo bado upo. Tunataka Tume Huru ya Uchaguzi ambayo ndani yake haina makada kama Mapuri ambaye alikuwa Mwenezi wa CCM"- @zittokabwe, Kiongozi wa Chama Mstaafu, @ACTwazalendo.

"Jana kuna rafiki yangu alikuja kwangu kupata naye futari. Akawa ananihadithia kuwa kuna jamaa amemuambia anishawishi nisigombee Ubunge Kigoma Mjini kwa sababu CCM hawatanipa. Nikasema ebo! kwani ni CCM au wananchi wanaotoa mbunge? Hapo ndipo tulipofika. Watu wa CCM wamefika pahala ambapo wanaweza kusema fulani hatutakupa"- @zittokabwe, Kiongozi wa Chama Mstaafu, @ACTwazalendo.

"Tunapigania thamani ya kuratasi ya kupigia kura. Karatasi za kupigia kura zisiwe kwenye mikono ya mabalozi, polisi au Maofisa wa Usalama wa Taifa. Mpiga kura aikute kwenye kituo na aiche kwenye kituo, isitoke nyumbani kwa mtu"- @zittokabwe.

Post a Comment

0 Comments