Na Mwandishi Wetu
Mbunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2020-2025) Ndugu Nagy Livingstone Kaboyoka amejiunga na ACT Wazalendo leo tarehe 28 Juni 2025. Ndugu Kaboyoka amepokelewa na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Ndugu Dorothy Semu pamoja na viongozi wa Ngome ya Wanawake na viongozi wengine wa Chama katika Ukumbi wa Hakainde Hichilema uliopo Makao Makuu ya Chama, Magomeni Dar es salaam.
Ndugu Kaboyoka amewahi kuwa Mbunge wa Kuchaguliwa wa Jimbo la Same Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA (2015-2020) kwa kumbwaga Anne Kilango Malechela wa CCM na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali PAC kwa Miaka 10 (2015-2025).
0 Comments