KAMISHNA BADRU ALA KIAPO CHA MAADILI



Na Mwandishi Wetu

Kamishna wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA), Bw. Abdul-Razaq Badru leo tarehe 28 Juni, 2025 ameungana na viongozi wengine walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungaano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kula Kiapo cha Maadili katika hafla iliyofanyia Ikulu Chamwino Dodoma.

Akitoa ujumbe wake mara baada ya kuwaapisha viongozi wateule, Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemtaka Kamishna Badru kusimamia kikamilifu shughuli za Uhifadhi, kulinda Ikolojia, Uwekezaji na Maendeleo ya Jamii. 

Dkt Samia amesema Ngorongoro ni Urithi wa Dunia hivyo ni lazima ilindwe kuhakikisha kwamba ikolojia yake inaimarishwa na kulinda rasilimali zilizopo na kuhakikisha kuwa  umaarufu wake haupotei. 

Amesema ana matumaini makubwa na Kamishna Badru kutumia maarifa yake, ujuzi na uzoefu wake katika kuisimamia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

Rais Samia  alimteua Bw. Abdul-Razaq Badru kuwa Kamishana wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro tarehe 26 Mei, 2025.

Post a Comment

0 Comments