Mjumbe wa Halmashauri wa Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam Idd Azzan akikabidhiwa fomu ya kuomba ridhaa ya Chama kugombea Ubunge Jimbo la Kinondoni.
NA MWANDISHI WETU
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam Idd Azzan amechukua fomu ya kutia nia kugombea Ubunge Jimbo la Kinondoni, Dar es Salaam.
Akizungumza lea Juni 29, 2025 baada ya kukabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama ch Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni Amos Richard katika Ofisi za CCM za Wilaya hiyo Azzan ameomba ridhaa Chama kimpitishe aweze kugombea nafasi hiyo.
Azzan ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo hilo, amesema alikuwa kimya Kwa muda Mrefu kwa sababu Jimbo lilikuwa tayari na Mbunge lakini Kwa sasa baada ya Miaka mitano sasa Jimbo liko wazi na Chama kimeweka Demokrasia ya kila mwenye nia kuchukua fomu.
0 Comments