MAFTAH AJITOSA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI



Masoud Hassan Maftah akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa fomu ya kutia nia kugombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi.

NA MWANDISHI WETU

KATIBU wa Diaspora Tanzania Masoud Hassan Maftah amechukua fomu ya kutia nia kugombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waandishi habari baada ya kukabidhiwa fomu hiyo katika Ofisi za CCM Wilaya ya Kinondoni Maftah amesema ameamua kuchukua fomu Kwa sababu ni mkazi wa Kinondoni.

"Mimi ninatia nia ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni, nakiomba Chama kiweze kunipa fursa hii ili niweze kuwatumikia Wananchi," amesema Maftah.

Kwamba anaamini kama atapatiwa ridhaa ya CCM kugombea nafasi hiyo atawatumikia vyema Wananchi wa Jimbo hio la akinondoni.

Post a Comment

0 Comments