Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) Sheikh Alhad Mussa Salum akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
NA MWANDISHI WETU
JUMUIYA ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) inatarajia kuzindua Kitabu cha 4R za Mama Julai 22, 2025 jijini Dar es Salaam.
Hayo yamebainishwa leo Juni 10, 2025 na Mwenyekiti wa JMAT Sheikh Alhad Mussa Salim akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam.
"JMAT imeandika Kitabu kinachokwenda kwa jina "4R za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuleta utulivu, Amani na Ujenzi wa mahusiano ya Kimataifa na Kitaifa. Uzunduzi huu utafanyika Siku ya Jumapili Tarehe 22/6/2025 katika Hoteli ya Serena Ukumbi wa Kivukoni kuanzia saa 01:00 hadi saa 4:00 usiku," amesema Sheikh Salum.
Kwamba Kitabu hicho kimeandikwa na Wanazuoni wa Dini zote mbili za Kikristo na Kiislamu pamoja na Wanazuoni wa Elimu Dunia, wakichambua dhana mbalimbali za R-NNE katika muktadha wa kidini, kisiasa na kijamii Nchini.
Katika hatua nyingine Sheikh Salum JMAT imeandaa MAatembezi ya Hiari ya Amani (MHA) 2025, yatakayolenga katika kuwaleta pamoja Watanzania kwa ajili ya kuweka jitihada kubwa katika kuhamasisha Amani na Maridhiano Nchini hususan kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025.
Kwamba matambezi hayo marefu yatakuwa ya wa km. 452 Kwa miguu, Kutoka Dar es Salaam mpaka Dodoma Kwa muda wa siku 20 kuanzia Juni 19 hadi Julai 9 Mwaka huu.
Sheikh Salum amesema kuwa Matembezi yatahusisha watembeaji 300 na yatazinduliwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Juni 19, 2025 na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Kwamba Matembezi yatapita katika vituo 20 vya Viwanja vya Mnazi Mmoja, Kiluvya, Misugusugu, Vigwaza, Chalinze Pera, Ubena Zomozi, Mikese, Morogoro Mjini, Mvomero, Wami Dakawa, Dumila, Maguha, Kiyegeya, Gairo, Kibaigwa, Mbande, Chamwino Ikulu, Nzuguni na Dodoma Mjini.
Amesema katika vituo hivyo vya Matembezi, vituo vinne vitakuwa na Mkutano ya hadhara, ya kuelimisha Wananchi na katika vituo nane, kutafanyika makongamano ya ndani ya Ukumbi/madarasa kuelimisha Wananchi.
Amebainisha kuwa Matembezi hayo yatafikia kilele na tamati Julai 9, 2025 katika shughuli kubwa itakayofanyoka katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Convention Center (JKCC) jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais Dkt. Samia.
Akizungumzia kuhusu maonesho ya Amani ya JMAT, katika sabasaba 2025, amewakaribisha Wananchi wote kushiriki maonesho ya Amani ya JMAT katika Banda la Karume katika mabanda ya maonesho ya biashara ya Kimataifa ya sabasaba Temeke, Dr es Salaam.

0 Comments