NA MWANDISHI WETU,KIBAHA
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe. Silvestry Koka kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025 hatimaye amejitosa kuchukua fomu kwa ajili ya kuendelea kutetea na kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo hilo katika uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika Mwezi Octoba mwaka huu lengo ikiwa ni kuendelea kushirikiana na wananchi katika kuwaletea chachu ya maendeleo.
Koka akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo amesema kwamba nia na madhubumuni yake makubwa ni kuhakikisha anaendelea kushirikiana bega kwa bega na wananchi wa Jimbo la Kibaha mjini katika suala zima la kusikiliza changamoto walizonazo ikiwa pamoja na kuwaletea maendeleo katika sekta mbali mbali.
Koka amebainisha kwamba katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ameweza kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo ikiwemo kufanikisha kwa kiasi kikubwa kuweka mikakati madhubuti na imara ambayo imeweza kusaidia kwa kiais kikubwa suala la kuipandisha hadhi Halmashauri ya Kibaha mjini kuwa Manispaa.
"Katika kipindi changu cha ubunge kwa kipindi cha miaka mitano ya ubunge wangu kwa kipindi cha mwaka wa 2020 hadi 2025 Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweza kutenga fedha nyingi ambazo zimeweza kuleta mabadiliko na maendeleo makubwa katika kutekeleza miradi mbali mbali ya kimaendeleo katika Jimbo la Kibaha mjini na kwamba lengo lake kubwa la kuchukua fomu ni kuendelea kuchochea maendeleo ,"amesema Koka.
Koka amebainisha kwamba ameamua kuchukua fomu ya kuendelea kutete kiti chake cha ubunge kwa lengo la kuweza kuendelea kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Kibaha mini kwa kipindi kingine cha mwaka wa 2025 hadi 2030 kwani suala la kuchukua fomu ni haki ya kimsingi ya mwanachama wowote.
"Mimi kama mwanachama wa chama cha mapinduzi na Mbunge mstaafu nimeweza kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Kibaha mjini kwa kipindi cha miaka 15 na katika kipindi chote hicho nimeweza kushirikiana bega kwa beega na wananchi wa kata zote 14 katika nyanja mbali mbali na kuleta mabadilko katika sekta ya maji, elimu, afya, miundombinu ya barabara pamoja na huduma za kijamii,"amebanisha Koka.
Katika hatua nyingine Koka amewashukiru kwa dhati wana chama wa chama cha mapinduzi(CCM) pamoja na wananchi wote kwa ujumla kwa kuweza kumwamini na kumpa ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi kilichopita cha mwaka wa 2020 hadi 2025 na kuahidi kuendelea kuwapa ushirikiano wa kutosha endapo akifanikiwa kurudi na kuweza kutetea katika nafasi yake ya Ubunge katika msimu ujao.
Kadhalika Koka amebainisha kwamba pamoja na kuchukua fomu ya kutetea nafasi hiyo atahakikisha anaendelea kuzingatia misingi iliyowekwa katika chama na kwamba hata asipopata nafasi ya kuteuliwa na kuchaguliwa kuwa Mbunge ataendelea kushirikiana bega kwa bega na wananchama wengine katika kukijenga na kukiimarisha chama na kuwapa ushirikiano kwa wale wote ambao watapata nafasi katika ngazi mbali mbali.
Kwa upande wake Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Issack Kalleiya amesema kwamba hali ya zoezi la uchukuaji wa fomu linakwenda vizuri katika hali ya amani na utulivu na kwamba hadi sasa jumla ya wagombea 10 wameshachukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi za ubunge wa jimbo la Kibaha mjini.
0 Comments