NA MWANDISHI WETU
MJUMBE wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Chama Oyster Bay, wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Aneth Masegese amechukua fumu ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya Udiwani Viti Maalum Kata ya Msasani.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, Masegese amesema kuwa amefanya hivyo ili kutia hamasa kwa wanawake wengine kujitokeza na kuchukua fomu kuomba kugombea nafasi mbalimbali.
"Nmeona ninafaa na ninaweza ndiyo maana nimeamua kuchukua hii fomu kama chama changu cha mapinduzi pia kitanipitisha itakuwa ni jambo jema na heshima kwangu na kwa wanawake wanaojiamini na kuthubutu," amesema Masegese.
Mgombea huyo amechukua fomu katika ofisi za Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni, ambapo amekabidhiwa na Katibu wa UWT wa Wilaya hiyo, Haziati Juma.
0 Comments