Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Chama Cha Mapinduzi kimeitaja hotuba iliotolewa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan wakati akivunja Bunge la 12 , imeleta matumaini mapya , kurudisha ari na kukua kwa haiba ya ustawi wa Kisiasa, kiuchumi ,kijamii na kidemokrasia nchini.
Vile vile,CCM kimekiri Rais Dk Samia amefanya juhudi kubwa,akitumia akili, nguvu za kulitumikia Taifa toka alipochukua kijiti kufuatia kifo cha mtangulizi wake Hayati Dk John Magufuli.
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi , Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis, ameiita hotuba hiyo ni kabambe iliothibisha uwezo alionao na utendaji wenye ufanisi wa Serikali yake .
Mbeto aliseema kupanda kwa takwimu za ukuaji uchumi, pato ghafi la Taifa ,ukusanyaji mapato ya ndani na deni la Taifa ikiwemo shilingi ya Tanzania kukua huku mfumuko wa bei ukishuka kuwa hayo ni mafanikio ya kujivunia .
Alisema mauzo ya bidhaa za uzalishaji w ndani nje ya nchi, Akiba ya Fedha za kigeni iliopo ,Akiba ya Hifadhi ya chakula , juhudi za kupambana n rushwa na dawa za kulevya , yamempa Rais na serikali yake heshima ya kipekee .
"Kupitishwa kwa idadi ya Miswada Bungeni na kuwa sheria. Kuwepo uhuru wa habari, Vyama vya Siasa kufanya shughuli zake na msikumo wa kupatikana katiba mpya siku zijazo ni umadhubutu wa Serikali yake" Aliswma Mbeto
Kuhusu uhuru wa mawazo , utoaji wa maoni, kusajili vyombo vipya vya habari ili kufanyakazi zao,ni fursa inayohimiza kasi ya uwajibikaji,kutanuka kwa wigo wa demokrasia na utendaji unaoleta tija na ufanisi.
Aidha , Mbeto aliyataja masuala yote hayo, si aghalab kuyakuta katika baadhi ya nchi duniani hususan Barani Afrika ,lakini chini ya uongozi wa Rais Dk Samia , yote yamewezekana .
"Hotuba ya Rais Dk Samia amekunjua mbawa za uongozi wake katika azma ya kuliongoza Taifa. Amejipambanua na kuonyesha umakini alionao katika kutumikia Taifa na wananchi wake" Alieleza Mbeto
Katibu huyo Mwenezi aliongeza kusema hotuba hiyo ya Mkuu huyo wa Nchi , imeelezea kwa kina na juhudi mbalimbali za kimaendeleo zizochukuliwa ikiwemo mikopo , kukua kwa deni la Taifa kutokana kupanda kwa thamani dola .
"Ilikuwa ni hotuba yenye msisimko yenye kila sababu ya kuungwa mkono na watanzania wote . Unapoyatazama maendeleo yaliostawi nchini kila Mtanzania anakiri awamu ya sita imetimiza wajibu wake" Alieleza.
Hata hivyo Mbeto aliitaja fomula ya RNne chini ya utawala wa Rais Dk Samia ,imeifanya serikali yake kuwa ni uongozi kidemokrasia na kiongozi anayefuata utawala wa sheria na kuenzi haki za binadamu .
0 Comments