NCAA YASHUKURU WADAU WA UTALII KUFANYA NGORONGORO KUWA KIVUTIO BORA AFRIKA



NA MWANDISHI WETU

Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA), Abdul-Razaq Badru, ametoa shukrani kwa Watanzania, wadau wa sekta ya utalii, na wageni wote waliotembelea hifadhi hiyo kwa kuiunga mkono kwa kupiga kura, na hivyo kuifanya Ngorongoro kutangazwa kuwa Kivutio Bora cha Utalii Barani Afrika kwa mwaka 2025.

Kamishna Badru amesema ushindi huo ni heshima kubwa kwa Tanzania na ni matokeo ya ushirikiano wa karibu kati ya mamlaka hiyo, wadau wa utalii, na jamii kwa ujumla. Aidha, ameahidi kwamba NCAA itaendelea kuimarisha huduma na kulinda urithi wa kipekee wa Ngorongoro ili kuvutia wageni wengi zaidi kutoka ndani na nje ya nchi.

Hifadhi ya Ngorongoro ni miongoni mwa maeneo ya urithi wa dunia yaliyo chini ya UNESCO, ikijivunia mandhari ya kuvutia, wanyamapori wa aina mbalimbali, na historia ya kipekee ya binadamu.

Post a Comment

0 Comments