NA MWANDISHI WETU
MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni Abbas Tarimba, amerejesha fomu ya kuomba ridhaa ya Chama chake kutetea nafasi yake ya Ubunge wa Jimbo la Kinondoni, Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 30, 2025 jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhi fomu hiyo, Tarimba amesema ametimiza wajibu wake wa kidemokrasia na haki yake ya kikatiba kama raia mwenye wajibu wa kushiriki katika uongozi wa Taifa kwa kugombea nafasi ya uongozi.
Hata hivyo ameeleza kuwa baada ya kurejesha fomu hiyo kinachobaki ni kusubiri taratibu nyingine za Chama ili kuamua nani atakayepatiwa nafasi ya kuliwakilisha Jimbo la Kinondoni.
Tarimba, amekabidhi fomu hiyo kwa Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Amos Richard.
0 Comments