Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti wa ACT Wazalendo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Ndugu Othman Masoud, amekutana na Msaidizi Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Prof. Luis G. Franceschi, katika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo jijini London, tarehe 16 Juni 2025.
Katika mazungumzo yao, Othman alieleza changamoto za kisiasa na kidemokrasia Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, huku akiishukuru Jumuiya hiyo kwa mchango wake wa kihistoria, ikiwemo Muwafaka wa 1999.
Prof. Franceschi alimhakikishia ufuatiliaji wa karibu wa hali ya kisiasa Zanzibar na Tanzania, na dhamira ya Jumuiya hiyo kuendelea kusaidia utawala bora.
Baada ya kikao hicho, Othman alitembelea Chatham House na kufanya mazungumzo na viongozi waandamizi wa taasisi hiyo, inayoongoza kwa utafiti wa sera za kigeni barani Ulaya.
Ziara hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa majukumu yake ya kikazi nchini Uingereza.

0 Comments