SHIRIKA LA ROOM TO READ LAJIZATITI KUWALINDA WATOTO WA KIKE DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI



NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 

Katika kukabiliana na kupambana na  vitendo vya ukatili kwa watoto wa kike wazazi na walezi wametakiwa kutambua nafasi zao hususani kwa watoto wa kike kwa kuwajengea uwezo kuzungumza nao kwa ukaribu kuhusiana na stadi za maisha. 


Akizungumza na waandishi wa Habarti mjini Kibaha wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Mhamasishaji Jamii Mwandamizi kutoka Shirika la Room to Read Rogathe Maturo amesema kila mzazi akisimamia nafasi yake matukioo ya ukatili yatapunguza.

Maturo amesema  kupitia mradi wa mtoto wa kike shirika hilo limekuwa likiwajengea uwezo wa kufanya maamuzi kwenye maisha yao huku kukiwa na vikundi ambavyo vinajadili changamoto wanazokabiliana nazo.

Alisema kupitia jamii kwenye maeneo ya miradi wamekuwa wakishikiana na kwa kufanya vikaonna matembezi ya kaya kujadili mamnbo mbalimbali ya watoto wa kike kuwakinga na ukatili kuwajengea uwezo wa kufanya maamuzi.

Naye Afisa mradi machapisho bora ya usomaji  katika mradi wa usomaji na maktaba kutoka shirika hilo Dickson Msuva alisema kupitia mradi huo kumekuwa na mabadiliko kwa wanafunzi wengi kupenda kusoma kwanbidii.

Msuva alisema kupitia mradi huo tayari shule zaidi ya 35 mkoa wa Pwani  zimenufaika na mradi wa usomaji na maktaba ambapo wanaendelea kushirikiana na maafisa elimu kuanzia ngazi ya kata kuangalia ufundishaji wa walimu.

Kakizunguimza katika maadhimisho hayo Kaimu katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Peter Billa aliwataka Wazazi, Walezi na Jamii kwa Ujumla kuwa walizi wa watoto ili kuhakikisha mtoto anakuwa katika mazingira bora.

"Yote yaliyoongelewa hapa ni muhimu sana kwa watoto wetu ila niseme tu mtoto anahitaji ulinzi, mtoto anahitaji kulindwa na kuhakikisha anaishi katika mazingira bora, ni wajibu wetu wazazi, walezi, na jamii kuhakikisha hilo", alisema Billa.

Pia alisisitiza wazazi kuepuka migogoro ambayo sio ya lazima na kugombana mbele ya watoto kwa kutumia lugha za matusi na vitisho ili kuepuka kuharibu saikolojia ya watoto ambayo itapelekea kufanya vibaya katika masomo pia anapokuwa shuleni. 

Aidha alisisitiza kukaa karibu na watoto na kutumiza majukumu kama Mzazi au mlezi ili kuweza kujua changamoto mbalimbali zinazozikabili watoto hasa masuala ya ukatili wa Kijinsia.

Kwa upande wake afisa maendeleo ya Jamii kutoka Mkoa wa Pwani Grace Tete alisema kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika vilitanguliwa na shughuli mbalimbali za kuelimisha jamii kuhusu haki za watoto na waliweza kuwafikia wazazi/walezi zaidi ya 2000 kwa kutembelea maeneo ya msoko mbalimbali yaliyopo Mkoa wa Pwani.

Aidha alisema serikali kupitia mpango wa Taifa wa kuzuia ukatili umetekelezwa na jumla ya watoto 150 waliofanyiwa ukatili wameweza kufikiwa  na kupatiwa huduma stahiki.

Post a Comment

0 Comments