KITIMLA AJITOSA KUWATUMIKIA WANANCHI JIMBO LA KIGAMBONI



#KAZIINAONGEA

Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mkazi wa Kigamboni, Sinan Seif Kitimla, amejitosa rasmi katika kinyang’anyiro cha ubunge wa Jimbo la Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Kitimla amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo Juni 28, 2025 ikiwa ni siku ya kwanza ya kuanza kwa zoezi la uchukuaji wa fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kupitia CCM nchini kote. Zoezi hilo linatarajiwa kufungwa rasmi Julai 2, 2025.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Kitimla amesema amejiandaa kuwatumikia wananchi wa Kigamboni kwa kuzingatia mahitaji yao halisi na kuhakikisha maendeleo jumuishi katika sekta mbalimbali. Kujitokeza kwake kugombea nafasi hiyo si kwa sababu ya kulinda mali zake, kwani yeye hana mali, bali ni kwa nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa Kigamboni.

Zoezi la kuchukua na kurejesha fomu linaendelea katika ngazi zote za chama huku wagombea wakihimizwa kuzingatia taratibu, kanuni na maadili ya uchaguzi ndani ya CCM.

*#KazinaUtuTunasongaMbele*

Post a Comment

0 Comments