Mkuruegenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Ephraim Mafuru akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Habari mbalimbali katika picha kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
NA MWANDISHI WETU
BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imesema wageni zaidi ya 500 kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki katika tuzo za 32 za kimataifa za kwa Kanda ya Afrika na Bahari ya Hindi ambapo Tanzania itakuwa Nchi mwanyeji.
Hayo yemebainishwa leo Juni 11, 2025 na Mkurugenzi Mtendaji wa TTB Ephraim Mafuru akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambaye amesema tuzo hizo zitafanyika Juni 28 mwaka huu na lengo lake ni kutambua mchango wa wadau wa utalii duniani.
“Uwepo wa tuzo hizi nchini ni jitihada za Rais Dk Samia Suluhu hassan tunapaswa tumpongeze Tuzo kama hizi ziliwahi kufanyika miaka ya nyuma ambapo hazikuwa kwa ukubwa kama ilivyo sasa," amesema Mafuru.
Mafuru ameeleza kuwa kuchaguliwa kwa Tanzania kuwe mwenyeji wa Tuzo hizo kwa nchi za Afrika pia kumetokana na ushindi wa Nchi katika tuzo zilizopita kwani iliongoza kwa kuwa na tuzo tano tofauti na nchi nyingine za Afrika katika tuzo hizi zilizofanyika mwaka jana nchini Kenya.
“Shughuli kama hii mwaka jana 2024 ilifanyika Mombasa kenya Tanzania ili shinda tuzo tano ambapo bodi bora ya utalii ya utalii Afrika ilichukua TTB,kivutio bora cha utalii Afrika ilikuwa mlima Kilimanjaro, hifadhi ya taifa bora Afrika ilikuwa Serengeti, kivutio bora cha safari Duniani sasa mafanikio haya hayaji tu hivi hivi ni kazi kubwa imefanyika ikiongozwa na Rais wetu," amebainisha Mafuru.
Ameongeza kuwa kampuni mbalimbali zinazojihusisha na utalii zitashiriki ambapo washiriki 38 kutoka sekta bifasi na 12 kutoka Serikalini watashiriki.
Ametumia fursa hiyo kuwaomba wadau wa Sekta ya utalii katika Mkoa wa Dar es Salaam kuchangamkia fursa za hafla hiyo katika kuwahudumia wageni hao.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli ya Johari Rotana ambaye ndio ‘Host’ wa tuzo hizo Ahmed Said amesema wao kama hoteli wamejipanga vyema kuhakikisha wanawahudumia vyema wageni wote watakaofika kwenye tuzo hizo.
Naye, Mkurugenzi wa Masoko kutoka Hospitali ya Shifaa Victoria Tarimo amesema wamejipanga vyema kuhakikisha wanatoa huduma za kimataifa katika kuwahudumia wageni hao ambao watapata changamoto za kiafya wakati wa tuzo hizo.
“Sisi tumejipanga vizuri na tunavifaa vya kisasa kabisa kwa ajili ya kuwahudumia na tutakuwa nao bega kwa bega kuhakikisha tunawapa huduma nzuri kwani tunavifaa vya kisasa na wataalam wa kutosha lakini pia tutakuwa na gari la wagonjwa kwa ajili ya dharura,” amesema.
Amesema Hospitali imejipanga kusapoti agenda ya Rais Dk Samia ya Tiba utalii kwa vitendo. Tuzo hizo zilianzishwa mwaka 1993 lengo likiwa kutambua mchango wa wadau walipo katika Sekta ya Utalii katika maeneo mbalimbali Duniani.





0 Comments