NA MWANDISHI WETU
Mjumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kata ya Makongo, Wakili Abbriaty Kivea, amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Udiwani wa Viti Maalum Kata ya Makongo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 29, 2025 baada ya kukabidhiwa fomu hiyo ameomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi kumpatia nafasi hyo ili kuwatumikia wananchi.
Mgombea huyo amechukua fomu katika ofisi za Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni, ambapo amekabidhiwa na Katibu wa UWT wa Wilaya hiyo, Haziati Juma.
0 Comments