
NA MWANDISHI WETU
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni Michael Wambura amechukua Fomu ya kuomba ridhaa ya Chama chake kugombea Ubunge Jimbo la Kinondoni, Dar es Salaam
Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 30, 2025 mkoani Dar es Salaam baada ya kukabidhiwa fomu hiyo amesema amechukua fomu hiyo kutimiza haki yake ya kikatiba.
Wambura, amekabidhiwa fomu na Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Amos Richard.
0 Comments