NDOSSI AJITOSA KUCHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE WA JIMBO LA KIBAHA MJINI



NA MWANDISHI WETU, KIBAHA 

Mmoja wa mwanachama wa chama cha  mapinduzi (CCM) amejitosa kuchukua fomu kwa ajili ya kuomba ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025.

 Mgombea huyo ambaye anafahamika kwa jina la  Godwin Ndosi amesema ameamua kuchukua  fomu ya kugombea ubunge katika Jimbo la Kibaha Mji ili aweze kuendeleza pale alipoachia mwenzake Silvestry Koka.

Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu hiyo  Ndosi amesema kuwa anatambua Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka amefanyakazi kubwa lakini na yeye anaingia kwa ajili ya kuendeleza pale ambapo Koka ameishia.

"Nimekuja hapa kuchukua fomu na lengo kubwa ni kuleta mabadiliko ya Kibaha Mjini hususani katika kuwaletea Wananchi maendeleo lakini natambua Mbunge Koka kafanya mengi na mimi nitaendeleza pale alipoishia na lengo ni kuwaletea wananchi maendeleo.

Post a Comment

0 Comments