WIZARA YA NISHATI YATAKIWA KUENDELEA KUWEZESHA UWEKEZAJI WA VITUO VYA MAFUTA VIJIJINI



#KAZIINAONGEA

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene ameiasa Wizara ya Nishati kuendelea kuweka mazingira wezeshi yatakayowezesha uwekezaji zaidi wa vituo vya mafuta vijijini.

Simbachaene amesema hayo Juni 17, 2025, jijini Dodoma wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Nishati katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali ambayo leo yamefunguliwa rasmi

" Wafanyabiashara wengi wanataka kuwekeza kwenye vituo vya Mafuta vijijini kwakuwa bado kuna uhaba wa vituo, hivyo angalieni masharti yanayowekwa kwenye uwekezaji yasiwe kikwazo kwenye huduma hii muhimu." Amesema Simbachawene

Pia, Simbachawene ameishauri Wizara kuongeza kasi ya upatikanaji wa Nishati Safi ya Kupikia Vijijini pamoja na kuhamasisha uwekezaji kwenye Nishati Safi ya Kupikia.

Vilevile, ameipongeza Wizara ya Nishati na  Taasisi zake kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuendelea kutoa huduma za Nishati kwa wananchi.

*#KazinaUtuTunasongaMbele*

Post a Comment

0 Comments