NA MWANDISHI WETU
KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Leyla Noor Hussein Guma amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama chake kugombea Ubunge Jimbo la Kawe, Dar es Salaam
Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 1, 2025 mkoani Dar es Salaam baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, Leyla amesema amechukua fomu hiyo kutimiza wajibu wake wa kidemokrasia.
Kwamba hii ni mara yake ya nne kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama chake ambapo alifanya hivyo mwaka 2010, 2015, 2020 na sasa 2025.
Leyla, amekabidhiwa fomu na Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Amos Richard.
0 Comments