KATIBU WA DIASPORA TANZANIA MAFTAH AREJESHA FOMU KUOMBA RIDHAA KUGOMBEA UBUNGE KINONDONI



Katibu wa Diaspora Tanzania Masudi Hassan Maftah akirejesha fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi kugombea Ubunge Jimbo la Kinondoni.

NA MWANDISHI WETU

KATIBU wa Diaspora Tanzania Masudi Hassan Maftah, amerejesha fomu ya kuomba ridhaa ya Chama kuwania ubunge Jimbo la Kawe wilayani Kinondoni, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 1, 2025 jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhi fomu hiyo, Maftah amesema ametimiza wajibu wake wa kidemokrasia na haki yake ya kikatiba kama raia mwenye wajibu wa kushiriki katika uongozi wa Taifa kwa kugombea nafasi ya uongozi.

Hata hivyo amesema kuwa pamoja na kurejesha fomu hiyo sio kwamba tayari ameshapitishwa kugombea bali anasubiri taratibu nyingine za Chama kupitisha mgombea.

Maftah, amekabidhi fomu hiyo kwa Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Amos Richard.

Post a Comment

0 Comments