UONGOZI WA MISS WORLD WAMTEMBELEA RAIS SAMIA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NAYE KIZIMKAZI


*● Tanzania Kuelekea Kuandaa Miss World 2026*

#KAZIINAONGEA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameongoza mazungumzo muhimu na Uongozi wa Kampuni ya Miss World Limited, ukiongozwa na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wake Julia Evelyn Morley, pamoja na Mshindi wa Miss World 2025 Opal Suchata Chuangsri kutoka Thailand na Miss World Africa Hasset Dereje Admassu kutoka Ethiopia.

Mazungumzo hayo, yaliyofanyika Julai 20, 2025 Kizimkazi, Zanzibar, yalihudhuriwa pia na Viongozi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Katika kikao hicho, pande zote zilijadili kwa kina nafasi ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya Kimataifa ya Miss World 2026, ikiwa ni fursa ya kuitangaza nchi Kimataifa kupitia Utalii, Utamaduni na Sanaa.

Mara baada ya mazungumzo hayo, Mshindi wa Miss World 2025 Chuangsri alionekana akifurahia mazingira ya Kizimkazi, Zanzibar.

*#KazinaUtuTunasongaMbele*

Post a Comment

0 Comments