Na Mwandishi wetu, zanzibar
Chama Cha Mapinduzi kimesifu mpangilio wa malengo katika Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2025 - 2050 kwa kuiitaja ni njia na ramani sahihi ya kufikia Maendeleo na jinsi kushughulika na changamoto za msingi katika Taifa
Pia kimesisitiza Dira hiyo imelenga kuiongoza Tanzania ielekee na kuwa nchi yenye uchumi imara, jumuishi na yenye kujenga nguvu ya ushindani.
Katibu wa kamati Maalum ya NEC Zanzibar , Idara ya Itikadi ,Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis, ameeleza hayo huku akisifu dhamira njema ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan itakayosukuma mbele ari ya maendeleo.
Mbeto alisema mikakati ya kujenga jamii yenye elimu, afya bora, makazi salama na mazingira endelevu, ni katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia ya nchi, huo ndio mpango na mkakati madhubuti .
"Dira ya Taifa ya maendeleo ilioziduliwa na Rais Dk Samia imebeba matumaini ya Watanzania. Ni Dira iliodhamiria kufikia mabadiliko na kuharakisha maendeleo ya kweli" Alisema Mbeto.
Aliitaja Dira hiyo itajenga msingi wa kukuza haiba ya utawala bora, kudumisha Amani, Usalama na Utulivu, ikiwa ni kukuza ustawi wa nguzo tatu muhimu na dhima ya kuinua maendeleo ya Taifa.
"Kujenga Uchumi jumuishi na shindani hapo mmeshajua kipi mnachokitaka . Mkiwapatia uwezo watu wenu utakaoweka msukumo wa maendeleo mmeshafanikiwa. Hata mkipanga mikakati ya kisera ya uhifadhi mazingira mmeshajiandaa kifikra na kisera" Alisema
Aliongeza kusema iii kufanikisha malengo hayo na mengine , Dira hiyo imezitaja sekta kipaumbele kama kilimo, Utalii, Viwanda na Madini.
"Pia kuna sekta ya uchumi wa Buluu, ubunifu na michezo, pamoja na huduma za kifedha zote zimetajwa kwa lengo la kuharakisha mabadiliko na kasi ya maendeleo " Alieleza
Pia Katibu Mwenezi huyo, alisifu Dira hiyo ya taifa kwa kuweka vichocheo muhimu kama usafirishaji fungamanishi, Nishati, Teknolojia, Utafiti na mageuzi ya kidijitali yatayochochea shime ya maendeleo kwa haraka.
"CCM kwetu sisi ni fahari kuwa na Dira ya Taifa makini hadi 2050 itaongozwa na Mpango wa Maendeleo wa Miaka 25. Kilichobaki ni usimamizi makini na utekelezaji mzima wa mipango ya pamoja" Alisema Katibu Mwenezi huyo.
0 Comments