NA MWANDISHI WETU
WAKILI Msomi Julieth Rushuli amerejesha fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea Ubunge Jimbo la Kawe, Dar es Saalam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 2, 2025 jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhi fomu hiyo ameomba Chama cha Mapinduzi kumpatia nafasi ili kuwatumikia wananchi.
Rushuli, amekabidhi fomu hiyo kwa Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Amos Richard.

0 Comments