WAZIRI JAFO KUWA MGENI RASMI MAONESHO YA MUHARRAM EXPO 2025, yanafanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.





NA MWANDISHI WETU

BARAZA Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania (BARAZA KUU)limesema Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maonesho ya mwaka huu ya Muharram Expo yanayoendelea viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Hayo yamebainshwa leo Julai 18, 2025 na Mwenyekiti Mtendaji wa Yusra Sukuk Sheikh Mohamed Issa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Sheikh Issa amesema maonesho hayo ni ya pili ya huduma za kifedha na kijamii yaliyopewa anuani ya "Mhuharram Expo) ikiwa ni ishara ya kuingia katika mwaka mpya wa Kiislamu ambapo Mwezi huu wa Muharram ndiyo mwezi wa kwanza katika Kalenda ya Kiislamu iitwayo kama Kalenda ya Hijria (Hijri Calendar).

"Kauli mbiu yetu ni "Muharram Expo: Onesha kujali jamii, toa huduma, sambaza amani". Ni maonesho yanayojumuisha shughuli mbalimbali za kifedha zisizo na riba kama vile huduma za kibenki, Vicoba na Saccos. Katika huduma. Katika huduma hizi utafahamishwa jinsi ya kuweka akiba, kupata mikopo au uwezeshwaji usio na riba," amesema Sheikh Issa.

Sheikh Issa ameeleza kuwa katika maonesho hayo pia watu watafahamishwa kuhusu huduma za Masoko ya Mitaji na Dhamana ikiwa ni pamoja na Uwekezaji wa Pamoja usio na riba kama vile Mifuko ya Uwekezaji Halal au Halal Funds, Hatifungani zisizo na riba zijulikanazo kama Sukuk, Hisa za Makampuni zilizokidhi Masharti ya Shari'ah hivyo kuwa Halal na jinsi ya kujichunga na Hisa zisizo Halal.

Sambamba na huduma za kifedha, piwa watapata maelezo ya huduma za kijamii kama vile uwekezaji wa wakfu, huduma za afya kama vile upimaji wa afya kutoka kwa jopo la madaktari wa maradhi mbalimbali, huduma za utoaji wa damu salama na huduma za msaada wa kisheria juu ya masuala mbalimbali kutoka kwa wataalam bobezi wa mambo ya kisheria.

Akizungumzia kuhusu huduma mtambuka zilizopo katika maonesho hayo Sheikh Issa amebeinisha kuwa kuna huduma za uuzaji wa vitabu mbalimbali vya kukuza uelewa na maarifa juu ya mambo mbalimbali pamoja na huduma za elimu za Chuo Kikuu kupitia Mtandao yaani Online University.

Kwamba kuna huduma ya Jeshi la Zimamoto wakitoa maelezo na maelekezo mbalimbali kuhusu masuala ya majanga ya moto na uokoaji na pia kuna huduma za Jeshi la Polisi kwa Usalama wa Raia na mali zao ambapo Trafiki wanatoa mafunzo na ushauri kwa bodaboda.

Amesema kwa ajili ya kujali afya za watakaofika katika eneo hilo, kuna gari la wagonjwa wa dharura (Ambulance) kwa ajili ya watu watakaohitaji huduma ya dharura ya kiafya itakapolazimu kukimbizwa hospitali.

Kwa upande wake Amiri wa Baraza Kuu hilo Sheikh Mussa Kundecha amesema kuwa wameamua kufanya maonesho hayo katika viwanja hivyo vya wazi vya Mnazi Mmoja ili kila mtu aweza kufika na kupata huduma anayohitaji.

Post a Comment

0 Comments