MKURUGENZI TUME YA TEHAMA AHIMIZA WATAALAM WA TEHAMA, Dkt. Mwasaga agusia Dira 2050



NA MWANDISHI WETU

MKURUGENZI mkuu wa Tume ya tehama nchini,Dkt Nkundwe Mwasaga,amesema bado Tanzania inahitaji wataalamu wa masuala ya tehama ili kuweza kuisaidia jamii kwenye mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

Dkt Mwasaga ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akifunga mafunzo ya siku tano ya usalama wa mitandao ,mafunzo hayo yaliwakutanisha maafisa mbalimbali kutoka Serikalini na sekta binafsi ambayo yalikuwa yanalenga kuwajengea uwezo wataalam hao katika maeneo ya usalama wa mitandao.

Dkt Mwasaga amesema katika dira ya mwaka 2050 inaonesha mahitaji makubwa kwenye tehama katika kuendesha uchumi kwenye sekta mbalimbali.

“Tukitaka kutengeneza Uchumi ambao upo salama,ili tuweze kufikia uchumi wa kutengeneza fedha za kigeni dola milioni moja hatuna budi kuwekeza juhudi kwenye kuwapata wataalamu”Amesema .

Amesema wataalamu hao wanahitajika wawepo kwenye ngazi za wilaya na vijiji ili waweze kusaidia jamii kwenye
uelewa wa masuala ya tehama na kusaidia hasa mapambano ya uhalifu wa mtandao.

Akizungumzia mafunzo hayo,Dkt Mwasaga,amesema mafunzo hayo ni ya siku tano yaliwakutanisha maafisa 33 kutoka sekta ya Umma ambayo yameandaliwa na Tume ya Tehama ikishirikiana na taasisi ya Korea kusini (KISA).

Amesema ujuzi walioupata watu hao 33 wataenda kuwapatia na wenzao wengine.

“Tunahitaji kuwa na wataalamu wengi ili kuwa na uchumi wa kidijitali kuongeza wawekezaji, watu kuwa huru kutumia mitandao yenye fursa mbalimbali.

Kwa upande wao wanufaika wa mafunzo hayo akiwemo,Afisa ulinzi binafsi kutoka kampuni ya simu ya TTCL,Liliani Chambili,ameipongeza Tume ya tehama kwa mafunzo hayo na kusema yamewajengea ujuzi kwenye utafiti ikiwemo kwenye taarifa za mtu zinapovuja.

Liliani ametumia nafasi hiyo kuiomba tume ya tehama kuongeza mafunzo hayo ili kuwajengea uelewa zaidi.

Post a Comment

0 Comments