RC KUNENGE AFUNGUA RASMI HOTEL MPYA YA KISASA YA MAYBORN KATA YA PICHA YA NDEGE


Na Victor Masangu,Kibaha

MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesema kuwa Serikali inaunga mkono uwekezaji unaozingatia vigezo vya kisasa hasa katika kukuza uchumi katika mkoa huo.

 Kunenge ametoa kauli hiyo Septemba 4,2025 wakati akifungua hoteli mpya ya The Mayborn iliyopo Mtaa wa Lulanzi Kata ya  Picha ya Ndege katika Manispaa ya Kibaha.

Akizungumza mara baada ya ufunguzi huo Kunenge amesema kuwa hoteli hiyo ni moja ya mipango ya kuhakikisha malengo ya kukuza uchumi na ongezeko la ajira kwa Watanzania linafikiwa.

Kunenge amesema uwekezaji huo ni wakimkakati kwani hoteli hiyo itawezesha wawekezaji ambao walikuwa wakilazima kuishi Dar es Salam sasa wamesogezewa kwa karibu.

"Wawekezaji wengi wanaowekeza Pwani wanakaa Dar es Salam sasa uwepo wa hoteli hii itasaidia na itafungua milango ya uchumi kwa hadhi ya Manispaa" amesema.

Mkurugenzi mtendaji wa  hotel hiyo Fikirini Mushi alisema kuwa alinunua ardhi mwaka 2009 na alianza ujenzi wa awali mwaka 2010 ambapo ujenzi huo ulidhaminiwa na Benki ya biashara ya NBC.

Alisema wakati wanajenga wamekabiliana na changamoto ya miundombinu ya barabara ambayo hadi sasa bado haijawa ya kuridhisha hasa nyakati za mvua hali ambayo inarudisha nyuma kasi ya ujenzi na hata utoaji wa huduma.

Alisema lakini ameendelea kuwa na matumaini na imani kwa Serikali yake sikivu na itaendelea kuboresha miundombinu ili kuchochea zaidi shughuli za kibiashara na uwekezaji.

Alisema hotel hiyo itatoa huduma mbalimbali ikiwemo malazi ,kumbi za harusi na mikutano pamoja na maeneo mengine ya biashara ambayo yatawapunguzia Wananchi adha ya kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma hizo.

Alisema faida za uwekezaji huo ni kutoa ajira zaidi kwa Wakazi wa Mkoa wa Pwani,kulipa kodi ya Serikali na kuvutia wawekezaji wengine.

Post a Comment

0 Comments