BARABARA ZAONGEZA UCHUMI RUVUMA, TARURA Ruvuma kutekeleza Miradi ya Bilioni 22 kwa mwaka 2025/2026




Na Mwandishi Wetu, Ruvuma

Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) mkoa wa Ruvuma umeendelea kunufaika na uwekezaji mkubwa wa Serikali katika miundombinu ya barabara, hatua inayochochea maendeleo ya kiuchumi, kilimo, na uhifadhi wa mazingira. 

Meneja wa TARURA mkoa  wa Ruvuma, Mhandisi Silvester Chinengo, amesema kwa mwaka wa fedha 2025/2026, mkoa huo unatekeleza miradi ya maendeleo yenye bajeti ya shilingi bilioni 22, ikiwa ni ongezeko kubwa kutoka bilioni 7 za awali.

“Kwa sasa, TARURA Ruvuma inasimamia mtandao wa barabara wenye urefu wa kilomita 7,147, ambapo kilomita 133.69 ni za lami, 1,651.8 ni za changarawe, na 5,360.6 ni za udongo. Takribani asilimia 70 ya barabara hizo zinapitika msimu wote, jambo ambalo limeleta mabadiliko chanya kwa wakulima na wafanyabiashara wa mkoa huo”.

“Barabara hizi zimekuwa mkombozi kwa wakulima. Mazao kama mahindi na kahawa sasa yanafika sokoni kwa wakati, bila kuharibika njiani na hivyo kuongeza uchumi kwa wakulima", amesema Mhandisi Chinengo.

Aidha, Meneja huyo amesema TARURA imefanya manunuzi ya mikataba 43 yenye thamani ya shilingi bilioni 12.1, na iko katika hatua za mwisho za kusaini mikataba hiyo.

Post a Comment

0 Comments