Na Mwandishi wetu, Dar es salaam
KUTOKANA na uvunjifu wa amani na uharibifu wa miundombinu uliojitokeza kwa siku nne hadi tano zilizopita kwa baadhi ya maeneo hapa nchini ,wadau mbalimbali wamejitokeza na kulaani vikali vitendo hivyo.
Wamedai kwamba hali hiyo haipaswi kujitokeza tena katika nchi yetu nakwamba haikuzoeleka kwa wananchi na kwenye macho ya watanzania kwa miaka mingi iliyopita.
wameeleza kwamba Tanzania ni kimbilio la wengi na ni kisiwa Cha amani na mataifa mbalimbali yana kimbilia nchini kutokana na amani ambayo ipo tokea enzi na enzi na hii ni tunu kwa Taifa letu
" Mataifa ya bara la Afrika na hata mataifa ya nje ya nchi ikiwemo Ulaya yamekuwa yakiitazama Tanzania kama kioo cha jamii katika suala zima la amani , utulivu,umoja na mshikamano ndio Nguzo kubwa kwa watanzania",
Hata hivyo wamesema kilichojitokeza Oktoba 29 hadi Novemba 2,2025 hakipaswi kujirudia kabisa kwani ukiacha uharibifu uliojitokeza lakini baadhi ya watanzania wamepoteza maisha jambo ambalo halijawahi kutokea wala kuzoeleka kwa wananchi kwani wamezoea kuona amani ikitawala nchini
Sambamba na hayo Miundombinu ambayo imejengwa kwa gharama kubwa zinazotokana na kodi ya watanzania imeharibiwa ,watu wamekatisha maisha yao kutokana na vurugu hizo lakini baadhi ya watanzania wamevunjiwa maduka yao,wameharibiwa mali zao kutokana na hali hiyo iliyojitokeza .
Kwa upande wake Mfanyabiashara mkubwa eneo la kariakooo, Shaban Kassimu lyomekyo amezungumzia hali ya uvunjivu wa amani iliyojitokeza kwa baadhi ya makundi ya watu kufanya vitendo visivyo kubalika , yeye kwa nafasi yake kama mfanyabiashara analipongeza sana Jeshi la polisi kwa kazi kubwa iliyofanya.
Shaban amesema kuwa Jeshi la Polisi chini ya IGP Camirius Wambura linastahili kupongezwa sana kwa kusimama imara kuhakikisha watanzania wanabaki salama lakini kubwa zaidi eneo la kariakoo ambalo linakusanya maelfu ya wafanyabiashara linakuwa salama katika kipindi chote Cha vurugu hizo.
Pia amesema unapozungumzia Jiji la Dar es Salaam ni lango la biashara maana yake unagusa moja kwa moja eneo la Kariakoo hivyo kitendo Cha Jeshi la Polisi kuimarisha Ulinzi katika kipindi chote Cha vurugu wanapaswa kupongezwa kwa nguvu zote
Shaban amefafanua kuwa Jeshi hilo hususani Kanda Maalumu ya Dar es salaam iliyopo chini ya Kamanda wa Polisi SACP Jumanne Murilo aliweza kupanga vijana wake kwa ustadi wa hali ya juu kiasi kwamba Kila lango la kuingia katika eneo la Kariakoo linakuwa na Ulinzi wa kutosha.
Amesisitiza kwamba eneo la Kariakoo ndio kitovu Cha biashara ambapo wafanya biashara wengi ndani na nje ya Dar es Salama wanakuja Kariakoo kufunga mizigo hivyo eneo hilo kama lingetikisika maana yake ni kwamba hata uchumi wa nchi ungetikisika kwa kiasi kikubwa mno.
"Hapa nichukue fursa hii kulipongeza tena na tena Jeshi letu la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama wa nchi yetu kwa namna walivyojipanga na kuhakikisha Kariakoo inabaki salama na hivi sasa wafanyabiashara wanaendelea na shughuli zao kama kawaida ."amesema Shaban
Angalia pale Kariakoo panabeba watu wangapi ,kwa maana ya wafanyabiashara wangapi alafu leo kama pangeharibiwa hali ingekuaje ?na ni kitu gani kingetokea?" ,amehoji ndugu Shaban .
Amesema Kariakoo ni lango kubwa mno la kibiashara ,wafanya biashara wakubwa wengi wapo eneo hilo hivyo ndio maana anasema anapongeza sana Jeshi kwa namna lilivyojipanga kuhakikisha eneo hilo linakuwa salama .
Ameongeza kuwa Jeshi walifanikiwa kuweka vizuizi katika eneo la magomeni kwa maana ya barabara ya Morogoro lakini pia Tazara kuingia barabara ya Uhuru inayotokea Buguruni hadi kufika kariakoo na Mivunjeni kwa barabara ya Kilwa hakuna mtu kuingia mjini kwa maana ya Kariakoo.
"Nataka nisema kazi kubwa imefanyika ,unajua Kariakoo kama nilivyosema uchumi wa nchi unategemea hapo kwa asilimia kubwa ,Kariakoo Kuna maduka makubwa ya vipodozi ,Kuna maduka makubwa ya nguo ,pia katika eneo la Jangwani kule kuna wauzaji wakubwa wa vifaa vya pikipiki na eneo la Gerezani kuna maduka makubwa ya vifaa vya umeme."amesisitiza
Niseme nampongeza Kamanda Murilo na Jeshi lake kwa ujumla kwa kazi kubwa na nzuri waliofanya kwa kipindi chote cha vurugu na hata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt .Samia Suluhu Hassan aliposema shughuli za wananchi zirudi kama awali siku Ile ya Novemba,3 mwaka huu kama Kariakoo ingeharibiwa ingekuwa haijasaidia kutokana na uhalisia wa kibiashara eneo hilo.
Kariakoo inapokea wageni kutoka nchi jirani kama vile Malawi,Zambia ,Burundi ,Kenya ,Uganda ,Rwanda ,wote hao wanakuja Kariakoo kufungasha bidhaa kwa ajili ya kupeleka katika nchi zao hivyo Kwa kifupi hali ingekuwa mbaya sana sana kama eneo hilo lingeathiriwa.
Lakini licha ya hayo bidhaa zote zinazotoka Nchini china kwa asilimia kubwa Kariakoo ndio kutovu chake kwa maana zinafikia hapo ndio zinasafirishwa kwenda katika mataifa mbalimbali hasa katika nchi zile ambazo zinatumia bandari ya Dar es Salaam
Shaban amesema kuwa licha ya uwepo wa wafanyabiashara wa kubwa lakini kundi kubwa la wamachinga wanaofanya shughuli zao katika Jiji la Dar es Salaam kwa asilimia kubwa wanategemea wafanyabiashara wakubwa kutoka Kariakoo hivyo kitendo Cha kuilinda Kariakoo Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya Usalama ni jambo kubwa mno wamefanya.
Mfanyabiashara huyu ambaye kwa asilimia kubwa biashara zake anazifanyia Kariakoo pia anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tamko lake alilotoa baada ya kuapishwa kuwa Rais wa kipindi Cha pili Cha awamu ya sita kwani kama asingefanya hivyo hali ingekuwa ngumu mno katika jamiii yetu.
Gharama za maisha ndani ya siku chache za vurugu zilizojitokeza maisha yalipaa sana kiasi kwamba watanzania wengi walilaani vikali vurugu hizo na waliosababisha vurugu hizo huku baadhi ya wananchi wakiomba watanzania kutochezea tena amani iliyopo na iliyodumu kwa miaka mingi
Watanzania hao walisema waasisi wa Taifa la Tanzania kwa maana Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Aman Abeid Karume walifanya kazi kubwa ya kuunganisha umoja ,mshakamano miongoni mwetu bila kubaguana kwa makabila ,rangi , wala jinsia ya mtu badala yake ni utanzania wetu tu.
Amesema pia viongozi hao waliotangulia mbele ya haki walisisitiza watanzania kuilinda amani na kwamba Tanzania ndio nchi yetu na wote wanaoizunguka ni jicho la utulivu wao na amani yao iko Tanzania na sio mahali pengine .
Hivyo nikiwa sehemu ya mtanzania niendelee kulipongeza Jeshi la Polisi na vyombo vingine vyote vya Ulinzi na Usalama katika nchi yetu kwa namna walivyorejesha amani ,Usalama katika Taifa na niwaombe watanzania wenzangu kilichotokea kimetokea na kamwe kamwe tusiruhusu tena hali hiyo amesisitiza Shaban
Amemaliza kwa kumshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuendelea kuwa mlezi na mzazi namba moja wa Taifa letu tunamuombea Kila lenye heri katika safari yake mpya ya uongozi wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu wabariki Watanzania

0 Comments