*Rc Makalla aahidi udhibiti wa wizi wa mita za maji mkoani Arusha
NA MWANDISHI WETU
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla leo Jumatatu Novemba 24, 2025 amekutana na kuzungumza na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Hamidu Aweso, akimueleza namna ambavyo anaridhishwa na utekelezaji wa miradi ya Maji Mkoani Arusha.
Katika Mazungumzo yao kando ya kumueleza Mkakati wa Mkoa wa Arusha katika kudhibiti wizi wa Mita za Maji unaofanywa katika baadhi ya maeneo, Mhe. Makalla amempongeza pia Waziri Aweso kwa kuaminiwa tena na Rais Samia Suluhu Hassan, akimuahidi ushirikiano katika kutekeleza na kusimamia sekta ya maji.
"Ni wazi kwamba uhodari wako, ubunifu wako na uchapakazi wako ndiyo umemshawishi Mhe. Rais kuendelea kukuamini na sisi kama wadau ambao tunazunguka katika maeneo mbalimbali tunaona kazi kubwa inayofanywa na Wizara ya Maji katika maeneo mbalimbali na hata hapa Arusha kazi nyingi zinafanywa Mijini na Vijijini na ninaridhishwa na namna ambavyo tunaendelea kushirikiana." Amesema.
Kwa Upande wake Waziri Aweso amemshukuru Mhe. Makalla kwa upendo na ushirikiano wake mkubwa, akimpongeza na kumuahidi pia kusimamia kikamilifu alama aliyoiacha katika Wizara ya Maji alipokuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji kwa mapambano yake makubwa ya kudhibiti Wizi na upotevu wa maji uliokuwepo katika kipindi hicho cha Uongozi wake.
0 Comments