Dar es Salaam
Serikali imevitaka vyombo vya habari vya kimataifa kuheshimu weledi, maadili na sheria za uandishi wa habari vinaporipoti masuala yanayohusu Tanzania. Kauli hiyo imetolewa Novemba 23, 2025 jijini Dar es Salaam na Msemaji wa Serikali kufuatia kuongezeka kwa taarifa zenye upotoshaji, uzushi na zisizo na uthibitisho wa kutosha.
Serikali imesisitiza kuwa licha ya kuwepo kwa uhuru wa vyombo vya habari, uhuru huo haupaswi kutumiwa vibaya kwa kuchapisha taarifa zisizo sahihi zinazoweza kuchafua taswira ya taifa. Imesema haipingi ukosoaji, ila inahitaji ukosoaji wenye ushahidi, uhalisia na unaozingatia taaluma.
Wadau wa habari wameunga mkono hoja hiyo, wakitaka Serikali iendelee kuboresha mazingira ya upatikanaji wa taarifa kwa waandishi wa ndani na nje. Wachambuzi wa diplomasia wameonya kuwa taarifa potofu zinaweza kuathiri uwekezaji, utalii na mahusiano ya kimataifa.
Serikali imerejea msimamo wake wa kulinda uhuru wa habari huku ikichukua hatua kwa watakaokiuka taratibu na kusambaza taarifa za kupotosha.
0 Comments