Na Beatus Maganja, Morogoro
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imeendelea kuonesha ubabe katika mashindano ya SHIMMUTA 2025 baada ya kutakata kwenye michezo miwili muhimu iliyochezwa leo Novemba 27, 2025 katika viwanja vya Kigurunyembe Mkoani Morogoro.
Katika mchezo wa mpira wa miguu, TAWA ilipambana vikali dhidi ya MSD kwenye pambano lililovuta hisia za mashabiki. Licha ya mchezo kuwa mkali, TAWA iliibuka na ushindi wa mabao 2–1, ushindi ambao umeifanya timu hiyo kuendelea kutamba kwenye kundi lake.
Kwenye mchezo wa mpira wa pete, malkia wa TAWA nao hawakuachwa nyuma. Waliingia uwanjani kwa kasi na nidhamu ya hali ya juu dhidi ya BOT na wakawashushia kipigo cha 34–21 katika mchezo uliotawaliwa na uchezaji wa kasi na umakini wa juu.
Kwa matokeo haya, TAWA inaendelea kujiimarisha zaidi na kuwa timu tishio kwenye michezo ya SHIMMUTA 2025 ikionesha dhamira ya kuhitimisha mashindano haya ikiwa kileleni.
0 Comments