WAKILI,MHE.JUDITH KAPINGA AKABIDHIWA RASMI OFISI YA VIWANDA NA BIASHARA




NA MWANDISHI WETU

Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Dkt.Suleman Jaffo leo tarehe 20 Novemba,2025 amekabidhi rasmi Ofisi za Wizara ya Viwanda na Biashara zilizoko Mtumba Mkoani Dodoma kwa Waziri mpya wa Viwanda na Biashara, Wakili.Mhe.Judith Kapinga .

Akizungumza wakati wa makabidhiano, Waziri,Wakili Kapinga amemshukuru Dkt.Jaffo kwa utendaji wake wa kazi katika kipindi chote cha Uongozi wake.

Waziri,Wakili.Kapinga ameahidi  atayaendeleza yote pale alipoishia Mhe.Dkt.Jaffo ili kuhakikisha azma na maono ya Mhe.Rais.Dkt.Samia Suluhu Hassan aliyonayo yanatimia katika kukuza Sekta ya Viwanda na Biashara.

Kwa Upande wake, Dkt.Jaffo amempongeza Wakili.Kapinga kwa kuaminiwa na kuteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara na kumhakikishia kumpa ushirikiano wakati wowote katika kufanikisha maono ya Serikali.

Hafla ya makabidhiano hayo,imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Wakili.Mhe.Patrobas Katambi ,Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Ndugu.Dkt.Ashil Abdallah na Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara.

Imetolewa na Ofisi ya Mbunge Jimbo la Mbinga Vijijini,leo tarehe 20.11.2025.

Post a Comment

0 Comments