NA MWANDISHI WETU
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, amesema kuwa mchakato wa kuwaachia watuhumiwa waliokamatwa kufuatia vurugu za Oktoba 29, 2025 unaendelea ambapo jumla ya watu 1,736 kati ya 2045 waliokamatwa wanatarajiwa kuachiwa huru mara tu baada ya taratibu zote za kisheria kukamilika.
Dkt. Homera ametoa kauli hiyo leo, Novemba 26, 2025, alipotembelea Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa madhumuni ya kujionea utendaji kazi na hatua zinazoendelea katika usimamizi wa mashtaka nchini.
“Hadi kufikia jana tarehe 25, Novemba jumla ya watuhumiwa 607 kati ya 1,736 wanaotakiwa kuachiwa tayari wameachiwa huru na wengine waliobaki wataendelea kuachiwa kadri taratibu za kisheria zitakapokamilika” amesema Dk. Homera.
Katika ziara hiyo, Waziri Homera aliambatana na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Zainab Katimba, Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Franklin Rwezimula, pamoja na viongozi na watendaji mbalimbali wa wizara hiyo.


0 Comments