WAZIRI WA ULINZI NA JKT AMTEMBELEA NA KUMJULIA HALI JENERALI MIRISHO SARAKIKYA




Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho (Mb) tarehe 23 Novemba, 2025 amemtembelea Mkuu wa Majeshi Mstaafu wa Kwanza Mstaafu, Jenerali Mirisho Sarakikya  nyumbani kwake Arumeru Jijini Arusha   kumsalimia na kumjulia. 

Waziri wa Ulinzi na JKT, Dkt Simeon Nyansaho, amefanya ziara hiyo ya kwanza kwa Jenerali Sarakikya  tangu ateuliwe kuwa Waziri wa Ulinzi na JKT na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Dkt Rhimo Nyansaho amemueleza  Jenerali Sarakikya kuwa Serikali na Wizara inatambua na kuthamini  mchango wa Wakuu wa Majeshi Wastaafu  Jeshini na Serikali na Serikali kwa ujumla, akamuahidi Jenerali Mstaafu Sarakikya ushirikiano wake. 

Kwa upande wake Jenerali Sarakikya amemshukuru Waziri wa Ulinzi kwa kumtembelea  na kumjulia hali na akamshukuru Mheshimiwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa  kumuamini na kumteua Dkt Simeon Nyansaho, kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Post a Comment

0 Comments