𝗧𝗨𝗧𝗔𝗘𝗡𝗗𝗘𝗟𝗘𝗔 𝗞𝗨𝗜𝗟𝗜𝗡𝗗𝗔 𝗧𝗔𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜𝗔 𝗡𝗔 𝗨𝗦𝗔𝗟𝗔𝗠𝗔 𝗪𝗔 𝗥𝗔𝗜𝗔 𝗡𝗔 𝗠𝗔𝗟𝗜 𝗭𝗔𝗢 - 𝗥𝗔𝗜𝗦 𝗗𝗞𝗧. 𝗦𝗔𝗠𝗜𝗔





Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 amehoji juu ya maoni ya baadhi ya watu kuwa nguvu zilizotumika kwenye kudhibiti vurugu zilizotokea Oktoba 29 (iliyokuwa siku ya uchaguzi mkuu) na kuendelea ilikuwa ni nguvu kubwa, akiuliza nguvu ndogo ambayo ingeweza kutumika ni ipi ambapo pia amesema dola haipo hivyo kwa kuwaacha baadhi ya vikundi vya watu kufanya vurugu na kuhatarisha amani ya Nchi.

Rais Dkt. Samia amesema serikali ya awamu ya sita anayoiongoza itahakikisha inailinda nchi na raia wake pamoja na mali zao kwa nguvu zote.

Rais Dkt. Samia ameyasema hayo leo tarehe 2 Disemba 2025 wakati akizungumza na Wazee wa mkoa wa Dar es salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa JNICC Jijini Dar es salaam.

Post a Comment

0 Comments