Halmashauri ya Wilaya ya Longido imejipanga kuhakikisha
Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, Awali na Darasa la Kwanza walioasililiwa kwa
muhuMa wa Masomo wa Mwaka 2026 wanaanza masomo Shule zinapofunguliwa Januari
13, 2025.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Longido Mhe. Thomas Ngobei akizungumza baada ya ziara ya siku mbili ya ameanza ziara ya siku mbili ya kukagua maandalizi ya upokeaji
wa wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, Awali na Darasa la Kwanza kwa muhula wa
masomo wa mwaka 2026 hususan kwa shule mpya wilayani humo iliyoanza Disemba 30 na kukamili leo
Disemba 31, 2025.
Amesema kwa maandalizi yaliyofanyika na yanayoendelea
kufanyika ni matumaini yake kuwa ifikapo Januari 13, 2026 wanafunzi wote
wanaostahili kuanza masomu muhula wa mwaka 2026 wataanza masomo yao bila
vikwazo vyovyote.
Hivyo ametumia fursa hiyo kuwahimiza wazazi kuhakikisha
watoto wao wanaripoti shule zitakapofunguliwa bila kukosa kinyume na hapo hatua
kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaokaidi.
“Tumetembelea shule, tumepita kuhakiki maandalizi ya mapokezi
ya wanafunzi kwa mwaka 2026. Longido tumejipanga na tupotayari kwa mapokezi ya
Wanafunzi,” amesema Mhe. Ngobei.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Afya na Maji
Mhe. Obedy Mollel amesema kuwa baada ya kutembelea shule hizo wameridhika na
maandalizi kwani wamehakikishiwa na wakuu wa shule kuwa wamejipanga kwa
mapokezi ya wanafunzi.
“Shule hizi tumejiridhisha kwamba wamejipanga kwa mapokezi ya
wanafunzi. Walimu wakuu wametuhakikishia wanafunzi wote watapokelewa na
kuendelea na masomo yao,” amesema Mhe. Mollel.
Aidha amewapongeza wananchi kwa kuunga mkono juhudi za
Serikali kwa kushirikiana na viongozi wa Kata na Vijiji kutatua baadhi ya
changamoto kwa kuchangia baadhi ya mahitaji ikiwemo viti, meza na vitanda kwa ajili
ya kuweka mazingira rafiki kwa wanafunzi shule zitakapofunguliwa.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido
Mhe. Peter Lekaneti ametumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi kuanza kutatua
changamoto zinapotokea na Serikali itakuja kuongeza nguvu ili kumaliza
changamoto hizo.
Katika siku ya kwanza ya ziara hiyo Mhe. Ngobei alijionea maandalizi
katika Shule Shikizi ya Laalaroi na Shule ya Sekondari Noondoto zilizopo Kata
ya Noondoto. Aidha, alitembelea Shule ya Sekondari Mundarara na Shule ya Msingi
Lesing’ita, zote zilizopo Kata ya Mundarara.
Kadhalika kwa siku ya pili ya ziara Mhe. Ngobei alitembelea Shule ya
Sekondari Kimokouwa, Shule ya Sekondari Kamwanga, Shule ya Msingi Kamwanga,
Shule ya Sekondari Sinya, Shule ya Msingi Sinya, Shule ya Sekondari ya
Wasichana Longido Samia pamoja na Shule ya Msingi Oltepes.
Katika ziara hiyo, Mhe. Ngobei aliambatana na Makamu Mwenyekiti wa
Halmashauri, Mhe. Peter Lekaneti; Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji,
Mhe. Obedy Mollel; Kaimu Afisa Elimu Sekondari, Bw. Mgonza Salehe; pamoja na
Kaimu Afisa Elimu Msingi, Bw. Mustafa Kaisi.
Kwa mujibu wa ratiba ya Wizara ya Elimu, Sayansi
na Teknolojia, shule za Awali, Msingi na Sekondari zinatarajiwa kufunguliwa
rasmi Januari 13, 2026.
0 Comments